Jumapili 28 Septemba 2025 - 07:55
Kamwe hatutaacha silaha za muqawama

Hawza / Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon katika sherehe za kumbukumbu ya mwaka wa kwanza tangia kupata shahada Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiuddin mjini Beirut alisema: “Ewe Nasrullah, kama ulivyotufundisha, kamwe hatutaacha silaha za muqawama.”

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Naeem Qasim, Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon, katika hotuba yake kwenye sherehe ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza ya shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin mjini Beirut, alisema: “Kwa vitendo tunaishi katika wakati wa ushindi mkubwa.”

Akimuelezea shahidi Nasrallah alisema: Njia ya Hizbullah ilianzishwa kwa fikra, roho na damu yako, na Palestina imepandwa mioyoni mwetu. Njia yako, ewe Nasrallah, ni ya milele; ingawa walilenga mwili wako, ila roho yako iko hai.

Sheikh Naeem Qasim, katika sehemu nyingine ya hotuba yake akimuelezea Msimamizi wa Mashahidi wa Muqawama, alisema: “Ewe Nasrallah, umeweka makazi mioyoni mwetu na umefanya muqawama kuwa na mizizi, na nuru yake imeangazia kote ulimwengu.”

Alisema: “Wewe umebadilisha sura ya eneo hili hadi muqawama huu ukazidi kusambaa katika ulimwengu. Ewe Nasrallah, kama ulivyotufundisha, kamwe hatutaacha silaha za muqawama. Ewe Nasrallah, ulikuwa mfadhili kwetu katika kutoa mahitaji ya mbele ya mapigano dhidi ya adui.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon akielekeza manebo yake kwa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na shahidi Safiuddin, alisema: “Mmeondoka mapema sana, lakini athari zenu zinaendelea; sisi tumebaki watiifu kwa ahadi yetu kwenu.”

Sheikh Naeem Qasim, akimkumbuka shahidi Karki miongoni mwa mashahidi wengine wa muqawama, alibainisha: “Aliunga mkono njia hii kutoka Syria na alishiriki katika vita vyote vya kuiunga Ghaza. Shahidi Karki aliomwomba Sayyid Hassan Nasrallah kuwa pamoja naye katika uendeshaji wa vita, basi alipokea medali ya shahada pamoja naye.”

Akaendelea kusema: “Tumesimama dhidi ya vita vya kimataifa ambavyo ndani yake utawala wa Kizayuni ulijaribu kumaliza muqawama ili kuandaa njia ya kuanzisha Israeli Kubwa.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon alisema: “Baada ya mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuuwa makamanda wa muqawama, adui alidhani tutang’olewa, lakini kwa uteuzi wa makamanda wapya wa Hizbullah, tulirejesha udhibiti wa mambo.”

Aliongeza kuwa: “Katika pambano la Ulya al-Bass tuliweza kuzuia msururu wa uvamizi wa adui, huku ikiwa tukio la Peyjer na kuuuwa makamanda katika nchi nyingine lingeweza kutupasua.”

Sheikh Naeem Qasim alibainisha kwamba: “Tuko mbele ya adui anayejaribu kumaliza muqawama, lakini katika kufikia malengo yake ameshindwa. Muqawama umeweza kusimama wenyewe na katika pambano la Ulya al-Bass ulipigana na adui na pambano hilo linaendelea.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon akatangaza kuwa tuko tayari kwa ulinzi ili kukabiliana na Israel, alisema: “Mandhari zinazoonesha (huzuni za umati wa watu kwenye sherehe za kumbukumbu za mashahidi wa muqawama) zinaonesha nguvu ya muqawama, hasa mazishi ya mamilioni ya viongozi wa muqawama.”

Aliongeza kuwa: “Tuliweza kubaki kwenye uwanja wa vita na tulipata kile ambacho wengine kwa siasa hawakuweza kutimiza; tulikipata kwenye uwanja wa vita.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon alisema: “Marekani na utawala wa Kizayuni ni hatari kwa Lebanon na muqawama, na kamwe hatutaruhusu kuondolewa kwa silaha ya muqawama; tutakabiliana nayo kwa vita kali.”

Akitaja kwamba utawala wa Kizayuni kamwe hautaruhusu Lebanon kuwa na utulivu, alibainisha: “Serikali ndio inayowajibika kusimamisha uvamizi, kuondoka kwa utawala wa Kizayuni, kuachilia huru wafungwa na kuanza ujenzi upya wa Lebanon.”

Sheikh Naeem Qasim, akisisitiza umoja wa kitaifa, alisema: “Dola yetu ya kitaifa itazuia kuishi kwa utawala wa Kizayuni ndani ya ardhi ya Lebanon. Lazima tukabiliane na vitisho tukitegemea rasilimali zetu na kupambana na ufisadi wa ndani. Lazima tufanikiwe kuwaletea uhuru wana Lebanon kutoka kwa watekelezaji wa ukoloni kwa kupitia muqawama.”

Alieleza: “Tunataka utekelezaji wa kifungu cha saba cha kipengele cha pili cha Mkataba wa Taif kuhusu uchaguzi wa bunge la taifa la kwanza, na tunataka uchaguzi wa bunge ufanyike kwa wakati uliopangwa. Lazima tujenge nchi yetu kwa msaada wa kila mmoja kwani ni ya wote wetu.”

Sheikh Naeem Qasim akaendelea: “Tunaunga mkono jeshi kwa ajili ya kukabiliana na adui mkuu wa Lebanon. Adui wa Kizayuni ni hatari kuu kwa wote.”

Katibu Mkuu wa Hizbullah Lebanon akimtumia salamu, kiongozi na serikali ya Iran alisema: “Kwa msaada wao walifanya muqawama uendelee katika njia yake.”

Akaongeza: “Tunaitumia salamu Yemen ambayo imelipa gharama kubwa kwa ajili ya kudumisha heshima na hadhi ya muqawama. Tunaitumia salamu Lebanon na muqawama wake, hasa Imam Musa Sadr aliyepuliza roho ya muqawama ndani yetu. Tunaitumia salamu harakati ya Amal na mbele yake Nabih Berri. Sisi na makundi mengine yanayopinga ukoloni tupo pamoja katika uwanja wa vita.”

Sheikh Naeem Qasim akaendelea: “Tunaituma salamu Tunisia kwa ajili ya kujitolea kwa umma wake kuisaidia Palestina na kwa wafuasi wa muqawama walioko kwenye uwanja.”

Akiwaelezea waliohudhuria alisema: “Ardhi hii ambayo damu ya watoto wenu imetelekezwa ndani yake, itawaondoa Wazayuni na maadui, na itakuwa ya wakazi wake pekee.”

Akiongea na wafuasi wa muqawama alisema: “Wanataka kupitia suala la ujenzi upya na sera potofu, kuifanya serikali yenu iwe katika msukosuko. Lakini hakuna upande utakaoweza kuwashinda; nyinyi mtashinda na adui atahindwa.”

Sheikh Naeem Qasim kwa wafuasi wa muqawama alibainisha kuwa: “Tutaendelea kuwa watiifu kwa ahadi yetu na tutaendeleza njia ya shahidi Sayyid Hassan Nasrullah.”

Mwisho wa ujumbe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha